Visitors Counter



web counter

TRANSLATE

Wednesday, 13 August 2014

faida za tangawizi kiafya

ZIJUE FAIDA YA KUTUMIA TANGAWIZI, HUTIBU MAGONJWA 72
Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi.
Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.
Tangawizi inatumikaje ?:
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga.
Nini Faida ya Tangawizi?
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.
Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.
Jinsi ya kuitumia kama Dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.
Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mubadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffeina ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini, Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katia juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.
Hutibu Magonjwa gani ?
  • Tangawizi husaidia yafuatayo:
  • Kuongeza hamu ya kula
  • Kupunguza kichefuchefu
  • Kutapika, kuharisha
  • Kisukari
  • Shinikizo la damu
  • Kuongeza msukumo wa damu
  • Kutoa sumu mwilini
  • Maumivu ya tumbo na
  • Gesi tumboni.

Sunday, 13 July 2014

faida ya karanga mwilini



ZITAMBUE FAIDA ZA KARANGA MWILINI Unaweza ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni pamoja na 1. Kuimarisha afya ya moyo 2. Hupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri. 3. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza shinikizo la juu la damu 4. Huponya magonjwa ya moyo 5. Hupunguza uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). (unashauriwa kula kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri). SHARE na wenzio wasome