TRANSLATE
Sunday, 31 January 2016
Tuesday, 12 January 2016
Happy mapinduzi day
MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohaed Shein akaikagua gwaride katika sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12,2016
Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.
Monday, 11 January 2016
Mwanamke Muislamu afurushwa mkutano wa Trump
Baraza la uhusiano mwema la kiislamu nchini Marekani limemtaka mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, kuomba msamaha kwa kuamrisha mwanamke wa dini ya kislamu kufurushwa kutoka kwa mkutano wake wa
kisiasa.
Rose Hamid alilalamikia wito wa bwana Trump wa kuweka marufuku ya muda kwa waislamu wanoingia nchini Marekani.
Wafuasi wa Trump walipoketi, mwanamke huyo alisimama kwa ukimya, huku akivalia vazi lililokuwa na maandishi, salaam. Nimekuja kwa amani.
Umati uliyokuwemo ulifanya kelele za kejeli na maafisa wa usalama wakamwondoa.
Bi Hamid mwenye umri wa miaka 56 na ambaye anafanya kazi ya huduma katika kampuni ya moja ya ndege ,baadaye aliamrishwa na afisa mmoja wa usalama kuondoka.
Alizomwa wakati alipokuwa akifurushwa katika mkutano huo
chanzo bbc
Subira Katika Msiba Wa Kwanza Jaza Yake Pepo
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ يَا ابْنَ آدَمَ: إن َصَبَرْتَ وَاحْتَسَبْتَ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الْأُولَى لَمْ أَرْضَ لَكَ ثَوابا دون الْجَنَّةِ)) ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Umaamah ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah عَزَّ وَجَلَّ Anasema: Ewe Mwana wa Aadam, utakaposubiri na ukategemea (thawabu) katika msiba wa mwanzo, sitoridhia kwako ujira chini (ila) ya Pepo)) [Ibn Maajah]
Sunday, 3 January 2016
Beautiful Hadith is about Spending Wealth
(Sahih Muslim, Book 31, Hadith 15)
Subscribe to:
Posts (Atom)