Visitors Counter



web counter

TRANSLATE

Monday, 21 March 2016

Mtoto Afariki Kwa Kukosa Matibabu..Wazazi Waliamini Maombi Pekee

Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Laela A, Ruti Sikapitaamefariki dunia baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali  kwamadai kuwa imani ya dhehebu lao haliruhusu waumini wake  kutibiwa hospitali.

 Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatu
huku akiwa anafungiwa ndani na  baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwa
hawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na  dawa za hospitali.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Laela, Didas Simtengui,alisema kuwa mtoto
huyo alikuwa anaumwa kwa siku tatu na hawakumpeleka hospitali badala
yake walikuwa wanazidisha maombi wakiamini kuwa atapona.

 Mmoja wa majirani, Musa Mwanakulya  alisema kuwa wao walikuwa hawamuoni
mtoto huyo akienda shuleni na wenzake na walijua anaumwa na ametibiwa
isipo kuwa maombi ni kitu cha kawaida na walikuwa wakisikia wanaomba
kila siku katika nyumba hiyo.

‘’tulikuwa tunasikia wakisali sana huku wakiwa wamejifungia ndani,
tulipo uliza walidai kuwa wanamuombea Ruti anaumwa lakini hawataki
kumpeleka hospitali wakidai kuwa mafundisho ya dini yao haya ruhusu
kutibiwa hospitali….waliendelea kumuombea mpaka akafariki
dunia’’…alisema.

Majirani walipopata taarifa kuwa mtoto huyo amefariki kutokana na wazazi wake kugoma kumpeleka hospitali, walikwenda kuvamia katika nyumba hiyo
wakitaka wawakamate wazazi hao ili nao wawaue.

 Kutokana na vurugu kubwa kuibuka ililazimu polisi wa kituo cha Laela
wafike katika eneo hilo na kuwatawanya watu waliokuwa na hasira kali
na kuuchukua mwili wa marehemu kwenda kuuhifadhi katika chumba cha
kuhifadhia maiti kilichopo katika kituo cha afya cha Laela na wazazi
wa mtoto huyo kuwaweka rumande ili kuwaokoa na wananchi wenye hasira
kali.

Ukiendelea Na Tabia Hizi Mafanikio Kwako Yatakuwa Ni Ndoto....

Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.

Wednesday, 16 March 2016

Habari Mbaya Kwa Wapaka Poda...Poda Zadaiwa Kusababisha Kansa

Kuna ne.no moja tu linaloweza kusemwa kwa sasa, kuwa tumekwisha, baada ya kubainika kuwa poda iliyotumika kwa miaka mingi nchini, ambayo ni maarufu kama Johnson’s Baby Powder inadaiwa kusababisha kansa ya kizazi inayoleta maafa ikiwemo vifo, Risasi Mchanganyiko lina taarifa kamili.

Taarifa zilizopatikana kupitia mitandao ya internet, zinadai kwamba kampuni inayotengeneza poda hiyo ya Johnson and Johnson ya Marekani, Februari 25, mwaka huu ilihukumiwa kulipa faini ya kiasi cha dola milioni 72 (sawa na shilingi bilioni 144) katika Mahakama ya Missouri kama fidia kwa mwanamke mmoja aliyefariki dunia kwa kansa ya kizazi iliyotokana na matumizi ya vipodozi hivyo.

Familia ya mwanamke huyo, Jacqueline Fox ilitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya mahakama kuridhika kuwa ugonjwa na kifo chake kilitokana na matumizi ya vipodozi hivyo kwa zaidi ya miaka 35, akitumia poda pamoja na losheni ya bidhaa hiyo.

Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson ilikabiliwa na tuhuma kwamba kwa miongo mingi, kwa lengo la kufanya biashara zaidi, haikuwaonya wateja wake kuwa miongoni mwa viungo vinavyotengeneza bidhaa hiyo, vinasababisha kansa. Zaidi ya kesi 1000 zimefunguliwa huko Missouri na 200 New Jersey, zote zikiilalamikia bidhaa hiyo.