Leo tujifunze namna is kutengeneza mkate wa baga
MIKATE YA BURGER:
Mahitaji:
🔸Unga wa ngano vikombe 4 1/2
🔸Hamira vijiko 2 1/4 vya chai
🔸Chumvi kijiko 1 1/2 cha chai
🔸Sukari vijiko 2 vya chakula
🔸Vanila 1/2 kijiko cha chai
🔸Maziwa kikombe 1
🔸Maji 1/2 kikombe
🔸Siagi (butter au margarine) 1/4 kikombe
🔸Yai 1
NAMNA YA KUPIKA:
1. Pasha moto maziwa, maji pamoja n siagi jikoni hadi siagi ipate kuyeyuka. Epua acha mchanganyiko upoe kidogo
2. Tia unga vikombe 2, chumvi, hamira pamoja na Sukari katika bakuli kubwa, koroga vizuri kisha tia mchanganyiko wa siagi pamoja na yai na koroga vizuri kuchanganya.
3. Endelea kutia unga ulobaki kidogo kidogo ukiendelea kuchanganya vizuri hadi ufanye donge.
4. Kanda donge lako hadi liwe laini kisha gawa vipande 12 na tengeneza maduara kisha panga katika tray ulopaka mafuta. (hakikisha unaacha nafasi kila baada ya bhanzi ili zisishikane wakati wa kuoka)
5. Binya kidogo juu kwa kutumia kiganja au ubapa wa glass kupata flat surface, funika na wacha zifure kwa muda wa nusu saa.
6. Washa ove joto 190-200°C. Mikate ikiumuka paka maziwa au mayai juu kisha nyunyiza ufuta kama utapenda.
7. Oka mikate yako kwa muda wa dk 12-18 au hadi ipate rangi nzuri na kuiva.
8. Toa katika oven kisha paka siagi juu ikiwa moto na itoe katika tray ipange katika wire ipate kupoa. Mikate ikipoa tayari kwa kula. Enjoy
9. Mikate hii utatumia kufanya burger aina zote na pia sandwich, lakini pia unaweza kuila plain tu kwa chai au kwa mchuzi na supu.