Swalah ya Dhuhaa ni kati ya sunnah za Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Nufair, kutoka kwa Abu Dar-daa na Abu Dharr, kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: amesema Allah Mtukufu, "Ewe mwanadamu Swali kwa ajili (kutafuta radhi) Zangu, rakaa (chache) mwanzo wa mchana (Dhuhaa) Mimi Nitakuwa tosha yako wakati wa jioni" (At-Tirmidhiy Hadiyth Namba 475, Abu Dawuud Hadiyth Namba 1289 na Shaykh Al-Albaaniy katika Ir-waul-Ghaliyl Namba 1465).