Visitors Counter



web counter

TRANSLATE

Friday, 13 October 2017

science&technology

Kwa nini fenesi linanuka sana?

Fenesi limesifiwa kuwa mfalme wa matunda katika Asia ya Kusini Mashariki, lakini linatoa harufu ya kipekee, ambayo baadhi ya watu wanaipenda na wengine wanaichukia. Je, harufu hiyo inatoka wapi?
Kikundi cha kimataifa kinachoongozwa na wanasayansi wa Singapore kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature Genetics la Uingereza ikisema wamechambua jeni kamili za fenesi, na kuthibitisha baadhi ya jeni zinazohusiana na harufu.
Watafiti wamepima jeni za fenesi aina ya Musang King, na kugundua kuwa fenesi hilo lina jeni elfu 46, ambazo ni mara mbili ya jeni za binadamu.
Kemikali muhimu inayounda harufu mbaya ya fenesi ni Sulfide inayoweza kugeuka kuwa hewa. Watafiti wamegundua kuwa baadhi ya jeni zinachangamka sana wakati fenesi linapoiva, na kulifanya fenesi kutoa harufu kali.
Mimea mingine pia ina jeni hizi, lakini jeni hizi zina nakala moja au mbili tu, na jeni za fenesi zina nakala nne, ambazo zinalifanya kutoa Sulfide nyingi zaidi.
Watafiti wanaona jeni hizi ni muhimu kwa fenesi pori, kwani harufu kali inasaidia kuwavutia wanyama kula fenesi na kueneza mbegu zake.

No comments:

Post a Comment