Visitors Counter



web counter

TRANSLATE

Friday, 8 November 2019

Today's Ayatat-Talaq 65:7

Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji.

Monday, 25 February 2019

Swalah Ya Dhwuhaa

Swalah ya Dhuhaa ni kati ya sunnah za Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Nufair, kutoka kwa Abu Dar-daa na Abu Dharr, kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: amesema Allah Mtukufu, "Ewe mwanadamu Swali kwa ajili (kutafuta radhi) Zangu, rakaa (chache) mwanzo wa mchana (Dhuhaa) Mimi Nitakuwa tosha yako wakati wa jioni" (At-Tirmidhiy Hadiyth Namba 475, Abu Dawuud Hadiyth Namba 1289 na Shaykh Al-Albaaniy katika Ir-waul-Ghaliyl Namba 1465).

Saturday, 21 October 2017

Treni ya umeme Tanzania

Treni Mpya Ya Kisasa ya umeme Tz, Dar-Dodoma Masaa Mawili Tu
Dar mwanza itakua masaa 8 tu
Mradi unaendelea kujengwa na kwa mujibu wa waziri alivyotembelea ni kuwa mradi huu unajengwa kwa haraka sana wanafanya kazi masaa 24
Gharama za usafiri zitakua nafuu mno yaani kama nusu ya nauli ya basi linaloenda sehemu husika
Huu mradi ukikamilika mpaka mwanza utakua umegharimu zaidi ya trilioni 7.5 za kitanzania

Tuesday, 17 October 2017

Tatizo la kukosa choo


Vyakula 5 Vinavyosaidia na Vinavyosababisha Tatizo la Kukosa choo

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.

Baadhi Ya Vitu Vinavyosababisha Tatizo La Kukosa Choo:

Kutokunywa Maji ya Kutosha
Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani
Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi
Unywaji wa maziwa kupita kiasi
Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi.


Vyakula Vinavyosaidia Kutibu Tatizo La Kukusa Choo

Tende
Maji
Kahawa Na Vinywaji Vingine Vya Moto
Ulaji Wa Matunda Au Saladi
Ulaji Wa Mboga Za Majani


Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo La Kukosa Choo Pia:

Ukiachia vyakula, ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo. Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako.
Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili

Friday, 13 October 2017

science&technology

Kwa nini fenesi linanuka sana?

Fenesi limesifiwa kuwa mfalme wa matunda katika Asia ya Kusini Mashariki, lakini linatoa harufu ya kipekee, ambayo baadhi ya watu wanaipenda na wengine wanaichukia. Je, harufu hiyo inatoka wapi?
Kikundi cha kimataifa kinachoongozwa na wanasayansi wa Singapore kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature Genetics la Uingereza ikisema wamechambua jeni kamili za fenesi, na kuthibitisha baadhi ya jeni zinazohusiana na harufu.
Watafiti wamepima jeni za fenesi aina ya Musang King, na kugundua kuwa fenesi hilo lina jeni elfu 46, ambazo ni mara mbili ya jeni za binadamu.
Kemikali muhimu inayounda harufu mbaya ya fenesi ni Sulfide inayoweza kugeuka kuwa hewa. Watafiti wamegundua kuwa baadhi ya jeni zinachangamka sana wakati fenesi linapoiva, na kulifanya fenesi kutoa harufu kali.
Mimea mingine pia ina jeni hizi, lakini jeni hizi zina nakala moja au mbili tu, na jeni za fenesi zina nakala nne, ambazo zinalifanya kutoa Sulfide nyingi zaidi.
Watafiti wanaona jeni hizi ni muhimu kwa fenesi pori, kwani harufu kali inasaidia kuwavutia wanyama kula fenesi na kueneza mbegu zake.